KILICHOJIRI HIP HOP SUMMIT 23 NOVEMBER 2014



Ijumaa 23 Nov 2014, wana hip hop na wapenzi wa wadau wa hiphop, walisikiliza maada mbalimbaali na kutoa michango ya mawazo. Kati ya waliotoa mada ni Profesa Mitchel Strumpf wa Chuo Kikuu cha dar es Salaam aliyetoa mada Hip Hop Identity and its Struggles Globally, ambapo aliweza kurudi nyuma kwenye historia kujaribu kuonyesha Hiphop ilitoka Afrika na imerudi tena, Kuna nyimbo kutoka Bukoba zilizorekodiwa kwenye miaka ya 50 ambazo ukisikiliza inashangaza kwani inafanana sana na Hiphop ya leo.
  
Pia alitoa maelezo mengi kuhusu kasheshe ambazo Hip hop inapitia katika sehemu mbalimbali duniani kutokana na tafsiri ya muziki huu. Maada nyingine ilitolewa na John Kitime mwanamuziki wa Kilimanjaro Band .
Problems and Challenges in the Tanzania Music Sector,
Maada ambayo iliongelea historia ya muziki na mapokeo katika Tanzania na matatizo ambayo muziki umepitia na unapitia mpaka wakati huu. Baadhi ya mambo ambayo aliyataja ni Rushwa katika tasnia hii, matatizo ya utekelezaji wa sheria ya Hakimiliki, mahusiano ya historia ya Kisiasa ya nchi hii na muziki na wanamuziki wake, nafasi ya serikali katika maendeleo ya muziki.

Maada nyingine ilitolewa na Charlotte Hill O'Neal aka Mama C aliyetoa maada “Tuangalie tulikotoka ili kuweza kusonga mbele.” Ambapo katika maada hiyo alitoa mifano ya jitihada za wana Hiphop wa kwanza wa Marekani, katika mazingira yaliyokuwa magumu ya kukosa nafasi ya kazi zao kusikika redioni , na wakati hakukuwa na uwanja huu mpana wa internet.  
Katika maada yake hii aliongelea kuhusu kituo cha SUA (Saving Underground Artists) kilichopo Arusha na jitihada zake za kuendeleza Hiphop. Mada nyingine iliyotolewa ni  JE WANA HIP HOP WAFANYE NINI ILI KUWEZA KUTOKA ambayo ilikuwa na maelezo mengi ya kuonyesha  na kushauri njia mbadala za kuwawezesha wana HIP HOP kutoka katika mazingira yaliyopo.




About the Author

HOT SWAHILI HIPHOP

Author & Editor

Has laoreet percipitur ad. Vide interesset in mei, no his legimus verterem. Et nostrum imperdiet appellantur usu, mnesarchum referrentur id vim.

0 comments:

Post a Comment

 

© 2015 - Distributed By Free Blogger Templates | Lyrics | Songs.pk | Download Ringtones | HD Wallpapers For Mobile