Graffiti are writing drawings that
have been scribbled, scratched,or painted illicitly on a wall or other surface
often within public view
Graffiti pia yaweza
tafsiri ujumbe kwa jamii aidha wa kisiasa au kijamii na ni usanii uliotegemea
uchorwaji husika wa staili tofauti. Graffiti imekuja sambamba na muziki
wa hip hop music, b-boying, na elementi zingine.
Vijana walianza kuandika
majina yao kwenye kuta mbalimbali mitaani kwa kutumia vipande vya mkaa na lengo
lilikuwa kuacha alama na aina hii ya
usanifu ulipewa jina “chata”, a Swahili slang term for graffiti. Staili ya
uchoraji kwa mkaa ilibaki hovyo hadi mapema miaka ya 2000s
pale msouth afrika kwa jina Zaki alipofanya jitihada za kuanzisha mchoro
Dar es Salaam july 2003. “CURE” ni mchoro wa kwanza katika barabara ya Old
Bagamoyo Mikocheni ila kwa Bahati mbaya ,ulifutwa na baadaye ulirudishwa lakini kinyumenyume na
kugeuzwa chini juu.
Tanzanian hiphop history in general,
inawataja WCT Crew, ni crew
inayojishughulisha na graffiti plus creative arts ambapo wao wameendeleza harakati za usanifu
michoro katika viunga mbalimbali vya jiji la Dar –es- salaam. WCT means WACHATA
ni kampuni halali, Mejah Mbuya ni
marketing personnel, Meddy ni procurement manager, Kalasinga,ni meneja ugavi na Local ni mbunifu mkuu. Jijini Mwanza kuna
Edo amabye amejikita kwenye kuchora tattoo, Yuzzo, and Mizani 86 wapo Moshi pia
wakiendeleza usanifu wa elementi hii muhimu ya HipHop.
WCT wamezidi pata attention Tanzania
sababu media zimeelewa kazi zao na haina ubishi kwamba wameweka misingi chanya
na imara kwa watu kwenye suala zima la GRAFFITI. WCT walifika office za East
Africa TV Dar-es-Salaam kwa ajili ya kutengeneza ubunifu tofauti katika kipindi
cha HOT MIX kinachoruka Monday-Friday,
5:00 na idea ilikuwa kuleta maudhui ya rangi tofauti tofauti na maandishi yatakayosomeka
kirahisi na iliwachukua takribani masaa
matano kumaliza kazi hiyo .
Tembelea
www.facebook.com/wachatacrew AU
www.wachatacrew.blogspot.com
Graffiti pia yaweza tafsiri ujumbe kwa jamii aidha wa kisiasa au kijamii na ni usanii uliotegemea uchorwaji.More onhttps://t.co/IbJBCAHl54— HotSwahiliHipHop (@HotSwahilHipHop) August 25, 2016
0 comments:
Post a Comment